Serikali imetoa Mahindi na Maharage kwa wahanga wa mafuriko Rufiji mkoani Pwani.
Wakizungumza na ITV mara baada ya kugawiwa msaada huo baadhi ya wananchi waliopata janga hilo la mafuriko wameelezea mazingira wanayoishi kwa sasa.
Mbunge wa jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa ambaye alishiriki ugawaji wa msaada huo amesema tani 100 za Mahindi zimetolewa na serikali na Maharage ni michango ya wabunge wa mkoa wa Pwani.
Katika jimbo hilo la rufiji kata 12 kati ya 13 zimeathiriwa na mvua hizo ambapo hekari 9000 za Mahindi zimeharibiwa pamoja na hekari 8000 za mpunga mazao ambayo yalikua yanaelekea kukomaa tayari kwa mavuno ambapo tani 1300 za chakula zinahitajika.
Katika tukio lingine waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera uratibu ajira na wenye ulemavu, Jenista Mhagama ametoa wiki mbili kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Rufiji atatue suala la Nuru Muhani mwenye ulimavu ambaye amekua akifanya kazi katika halmashauri hiyo kwa miaka tisa lakini hivi karibuni malipo yake ya kila mwezi yameanza kupunguzwa.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni