Zaidi ya vijiji 50 katika kata 15 Muleba mkoani Kagera hazina zahanati wala vituo vya afya...


Zaidi ya vijiji 50 katika kata kumi na tano za wilaya ya muleba mkoani Kagera hazina zahanati wala vituo vya afya katika kipindi cha miaka 55 ya uhuru hali inayosababisha vifo vya mama na mtoto kwa kukosa huduma huku wengine wakilazimika kutembea umbali mrefu wa kilometa 40 hadi 60 kufuata huduma katika vituo vya afya na zahanati za mashirika ya dini.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wananchi wa kata kumi na tano za wilaya ya Muleba ambazo hazina huduma ya afya katika kipindi cha miaka 55 ya uhuru katika mahojiano maalumu juu ya upatikanaji wa huduma za afya vijijini wamesema kuwa ukosefu wa huduma katika maeneo yao wazee, mama na mtoto hupoteza maisha kutokana na umasikini unaowakabili kwa kushindwa kukodi magari na pikipiki ambazo zinatoza gharama kubwa kusafirisha wagonjwa kutokana na uchakavu wa miundombinu ya barabara iliyopo vijijini.
 
Akijibu malalamiko ya wananchi kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Muleba, afisa mipango wa wilaya hiyo Bw.Rabson Magesa amekili kuwepo kwa huduma duni za afya vijijini na kusema kwamba wilaya ya muleba imeanzishwa mwaka 1975 hadi sasa haijajenga hospitali ya wilaya kwa kutegemea hospitali za mashirika ya dini na kwamba ili kutekeleza azima ya serikali kila wilaya kuwa na hospitali zaidi ya shilingi bilioni kuni na tatu zinahitajika.






Source:ITV












































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..