Kenya yapata vifaa vya kisasa vya polisi..

uhuru azindua vifaa
uhuru azindua vifaa.



Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, siku ya Jumatatu alizindua rasmi vifaa vya kisasa vya kutumiwa na idara ya polisi nchini humo. Vifaa hivyo vilikuwa ni pamoja na magari yaliyo na silaha ambayo alisema yatatumiwa katika maeneo yanayokumbwa na ukosefu wa usalama nchini humo.

Akizungumza mjini Nairobi alipowakabidhi rasmi maafisa wa ngazi za juu vifaa hivyo, Kenyatta alisema hatua hiyo itawawezesha maafisa wa polisi kutotegemea vifaa vya jeshi la taifa kila kunapotokea hali ya taharuki inayohitaji polisi kuingilia kati.
"Ununuzi wa vifaa hivi ni hatua muhimu katika kupambana na utovu wa usalama," alisema rais Kenyatta.
Haya yanajiri takriban wiki tatu tu baada ya wanajeshi ambao idadi yaka bado haijajulikana kuuawa baada ya shambulizi lililotekelezwa na magaidi ya Al Shabaab katika kambi ya El-Ade, nchini Somalia.







SOURCE:VOA










































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..