Klabu Ya Simba Imekubali Kipigo Cha Bao 2-0 Kutoka Kwa Watani Wao Yanga..
Dakika 90 za Mtanange wa Watani wa Jadi, Simba na Yanga zimemalijika jioni hii hapa uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam kwa kutoka kifua mbele kwa timu ya Yanga baada ya kuchapa Simba bao 2-0. Magoli ya mchezo huo yametiwa kimiani na washambuliaji Donald Ngoma (Dakika ya 38 kipindi cha kwanza) na goli la pili limefungwa na Amissi Tambwe (Dakika ya 34 kipindi cha pili) na kufanya matokeo kubaki hivyo hadi mwisho wa mchezo.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Donald Ngoma (11) akimpiga chenga Golikipa wa Timu ya Simba, Vicent Angban na kupachika bao la kwanza kwa timu yake wakati wa Mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Yanga na Simba, uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.Yanga imeshinda Bao 2-0.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Donald Ngoma akishangilia Goli aliloipatia timu yake, wakati wa Mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Yanga na Simba, uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.Yanga imeshinda Bao 2-0.
Adbi Banda akiwaungia mkono mashabiki wa Simba mara bada ya kutolewa nje ya mchezo kwa kadi nyekundu na mwamuzi Jonesi Rukyaa kufuatia kuoneshwa kadi mbili za njano
MATOKEO YA VPL-LIGI KUU VODACOM
Jumamosi Februari 20
Yanga 2- 0Simba
Mgambo JKT 1 -1 Tanzania Prisons
Stand United 1-1 JKT Ruvu
Mbeya City 0-3 Azam FC
Toto Africans 1-1 Kagera Sugar
Source:Lindiyetu.com
Maoni
Chapisha Maoni