Mapacha watenganishwa salama Uswizi...
Watoto Maya na Lydia wakiwa hospitalini kabla ya kutenganishwa.
Madaktari nchini Uswizi wanasema kuwa wameweza kuwatenganisha watoto mapacha wa kike wa siku nane waliozaliwa huku viungo vyao vikiwa vimeshikana, wanaoaminiwa kuwa wachanga zaidi kuwahi kutenganishwa.
Mapacha hao, waliozaliwa mwezi Disemba walikua wameungana kwenye maini na kifua.
Maya na Lydia baada ya upasuaji wa kuwatenganisha kufanikiwa.
Vyombo vya habari vya Uswis vinasema kua mpango wa awali wa madaktari ulikua ni kuwatenganisha baada ya miezi kadhaa, lakini walisogeza mbele tarehe ya upasuaji wao baada ya kila mmoja wao kupata hali inayotishia uhai wao. Imeripotiwa kua mafanikio ya upasuaji huo yalikua ni ya 1% .
Mapacha hao wanaoitwa Lydia and Maya, walizaliwa wiki nane kabla ya muda kamili wa kuzaliwa katika hospitali ya Inselspital katika mji wa Bern, sambamba na mapacha wengine watatu waliozaliwa wakiwa wametengana na wenye afya.
Mmoja wa mapacha hao alikua na damu nyingi na shinikizo la damu.
Lydia na Maya kwa pamoja walizaliwa wakiwa na uzito wa kilo 2.2 kwa pamoja. Mmoja wao alikua na damu nyingi zaidi, na shinikizo kubwa la damu, huku mwingine akiwa hana damu ya kutosha.
Ilichukua muda wa saa tano kwa Jopo la madaktari 13 waliobobea kukamilisha jitihada za kuwatenganisha mapacha hao mnamo tarehe 10 Disemba.
SOURCE:BBC
Maoni
Chapisha Maoni