Wazalishaji sukari wadai usambazaji sukari unahujumiwa na kutengeza uhaba.



Sakata la kupanda bei ya sukari limechukua sura mpya baada ya umoja wazalishaji wa Sukari kudai kuwa kuna njama za baadhi ya wafanyabiashara wakubwa ambao mianya yao ya uingizaji wa sukari kutoka nje ya nchi imezibwa hivyo wameanza kuhujumu sukari ya ndani.

Mwenyekiti wa umoja wa wazalishaji hao wa sukari balozi Ami Mpungwe amesema wana uhakika njama za wafanyabiashara hao hazitafanikiwa kwani bei halisi ya Sukari ambayo inapaswa kuuzwa kwa rejareja haitakiwi kuzidi elfu mbili kwa kilo moja.
 
Naye kaimu mkurugenzi mkuu wa bodi ya Sukari Abdul Mwankemwa amesema kuna wafanyabiashara ambao wamehodhi sukari katika maghala kwa lengo la kuifanya iwe adimu na hivyo bei yake kupanda.
 
Kuhusiana na kwanini bei ya sukari kutoka nje ya nchi kuuzwa kwa bei nafuu kuliko ile inayozalishwa ndani ya nchi mmoja wa wazalishaji hao wa Sukari Seif Ali Seif kutoka kiwanda cha Sukari Kagera anaeleza.
 





Source:ITV












































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..