KUZIONA SIMBA NA YANGA NI TSH. 30,000
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) Jumamosi kati ya watani wa jadi Simba dhidi ya Yanga SC utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku kiingilio cha chini kikiwa ni Sh. 7,000.
Kiingilio cha juu cha mchezo huo kitakua Sh. 30,000 kwa VIP A, 20,000 VIP B & C, Sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya machungwa (Orange), na Sh. 7,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani.
Tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa siku ya Ijumaa saa 2 kamili asubuhi katika vituo vya TFF (Karume), Buguruni Olicom, Ubungo Oilcom, Kidongo Chekundu (Mnazi Mmoja), Posta (Agip), Dar Live (Mbagala), Uwanja wa Taifa, Makumbusho Stand, Kivukoni Ferry.
Mchezo huo utachezeshwa na waamuzi wote wenye beji za FIFA, mwamuzi wa katikati Jonesia Rukyaa (Kagera), akisaidiwa na Josephat Bulali (Tanga), Samwel Mpenzu (Arusha), mwamuzi wa akiba Elly Sasii (Dar) huku Kamisaa wa mchezo huo akiwa Khalid Bitebo (Mwanza).
Ligi hiyo ya Vodacom itaendelea Jumamosi kwa michezo sita, Yanga na Simba (Taifa), Mbeya City na Azam (Sokoine), Stand United na JKT Ruvu (Kambarage), Toto Africans na Kagera Sugar (CCM Kirumba), Mgambo Shooting na Prisons (Mkwakwani) na Majimaji FC na Mtibwa Sugar (Majimaji).
Jumapili ligi hiyo itaendelea kwa michezo miwili, Mwadui FC na Coastal Union uwanja wa Mwadui Complex, huku Ndanda FC wakicheza dhidi ya African Sports uwanja wa Nagwanda Sijaon mjini Mtwara.
SOURCE:Mtembezi.com
Maoni
Chapisha Maoni