Obama kuhakikisha islamic state hawapigi kambi nchini Libya...
Raisi wa Marekani, Barack Obama ameapa kuhakikisha wanajihadi wa islamic state hawapigi kambi nchini Libya na kuongeza kuwa marekani itachukua hatua stahiki pale inapostahili.
Raisi Obama amebainisha kuwa kwa ushirikiano na mataifa mengine yanayopambana dhidi ya wanajihadi wa IS marekani itahakikisha wanakosa fursa ya kujikita nchini Libya.
Libya sasa inatimiza miaka mitano tangu mapinduzi ya kiarabu yaliyomuondoa madarakani aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo marehemu, Kanali Moamer gadaffi huku wakishuhudia mji wa kiongozi huyo ambao una bandari muhimu jirani na eneo la uchimbaji mafuta likitumiwa kama vyanzo vya mapato vinavyosaidia kundi la IS.
SOURCE:FOCUS MEDIA
Maoni
Chapisha Maoni