Matokeo ya Uchaguzi mkuu nchini Uganda yaanza kutolewa..

Uchaguzi mkuu nchini Uganda unafanyika leo, wengi wakiangazia sana uchaguzi wa urais ambapo kuna jumla ya wagombea wanane.
Mwanamke ni mmoja, Maureen Kyalya.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahidi kwamba matokeo yatakuwa tayari katika kipindi cha saa 48 baada ya kufungwa kwa vituo saa kumi alasiri.
Baada ya hapo, tume inatarajia kuwa ikitangaza matokeo ya urais baada ya kila saa mbili.
Mwenyekiti wa tume Badru Kiggundu aliambia wanahabari Jumatano kwamba huenda wakakosa kutoa matokeo mwendo wa saa thenashara leo lakini baada ya hapo watawapasha watu kuhusu matokeo kila baada ya saa mbili kupita.
Kituo cha taifa cha kuhesabia na kutangazia matokeo kinapatikana katika uwanja wa Mandela, Namboole eneo la Bweyogerere wilayani Wakiso.
Ili kutangazwa mshindi, mgombea anafaa kupata asilimia 50 ya kura zilizopigwa na kura moja juu. Hili likikosa kufanyika, kunafaa kuwa na duru ya pili ya uchaguzi ikishirikisha wagombea wawili waliopata kura nyingi zaidi.

1. Wagombea urais ni kina nani?

Ndio hawa hapa:
  • Abed Bwanika – Peoples Development Party
  • Amama Mbabazi – Go Forward
  • Benon Biraaro - Mgombea huru
  • Joseph Mabirizi- Mgombea huru
  • Kizza Besigye – Forum for Democratic Change
  • Maureen Kyalya – Mgombea huru
  • Venansius Baryamureeba - Mgombea huru
  • Yoweri Museveni – National Resistance Movement

2. Wapiga kura ni wangapi?

Kuna wapiga kura 15,277,196 waliosajiliwa nchini Uganda, na vituo 28,010 vya kupigia kura

3. Maeneo Bunge ni mangapi Uganda?

Kuna maeneo bunge 290 nchini Uganda.






SOURCE:Focus Media



































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..