Tukio la ujambazi Mbagala watu saba wameuawa akiwemo askari polisi mmoja,askari binafsi wawili na raia jijini Dar es Salaam.
Watu saba wakiwemo majambazi watatu wameuawa baada ya kutokea kurushiana risasi kati ya majambazi na Polisi kabla na baada ya majambazi hao kuvamia tawi la Access Benki lililopo Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi katika kanda maalum ya dar es salaam kamishina simon siro amesema majambazi 12 wakiwa katika pikipiki sita walivamia benki hiyo kwa nia ya kuiba fedha jaribio ambalo kwa kiasi kikubwa halikufanikiwa.
Amesema mbali ya majambazi watatu kuuawa,pia Polisi mmoja,askari wa kampuni binafsi ya ulinzi na raia wawili nao waliuawa katika tukio hilo ambapo majambazi walizitelekeza pikipiki zao na kuchanganyika na raia na baadaye kudaiwa wamekimbilia katika msitu wa Kongowe unaotenganisha mkoa wa DSM na Pwani.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Charles Kitwanga amesema mara baada ya mkutano huo na waandishi wa habari atawasiliana na waziri wa ulinzi ili wapatikane askari kutoka JWTZ kusaidia msako wa majambazi ambao wanadaiwa kujificha katika misitu inayotenganisha mikoa hiyo miwili.
Nao waendesha pikipiki wametakiwa kuwa wavumilivu kwani kuanzia sasa msako maalum unaendelea kuwabaini wahalifu ambao wengi wao hutumia Pikipiki.
Source:ITV
Maoni
Chapisha Maoni