Serikali imewasilisha bungeni mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa taifa 2016/7.



Serikali imewasilisha bungeni mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa taifa 2016/7 na muongozo wa kuandaa mpango na bajeti ya serikali kwa mwaka 2016/7 ambapo imebainisha vipaumbele vyake vitano ikiwemo sekta ya viwanda huku ikitegemea kutumai zaidi ya shilingi tirilioni 22 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo.

Mpango huo umewasilishwa na waziri wa fedha na uchumi Mh Dk Philip Mipango ambapo amesema sekta ya viwanda itapewa msisitizo mkubwa zaidi.
 
Wakichangia mpango huo baadhi ya wabunge wamesema umekuwa mzuri japo yapo baadhia ya maeneo ambyo inaonekana serikali iliyasahau na hivyo kuna haja ya kuuboresha zaidi ili uweze kuwa na tija.
 
Kwa upande mwingine baaadhi yao wamesema watendaji wa serikali wanapaswa kuongeza kasi ili mipango iliyobainishwa iweze kutekelezwa lakini kama haitakuwa na hivyo ni dhahiri kuwa mpango huo hautalisaidia taifa. 
 
Awali bungeni hapo kabla ya kuwasilishwa kwa hoja hiyo na Mh waziri wa fedha kulitokea mvutano wa kikanuni na hatimaye kanuni zikatenguliwa na bunge likakaa kama kamati ili kuweza kuijadili hoja hiyo.
 







SOURCE:ITV
















































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..