Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2015

PICHAZ: Hizi ni baadhi ya mali za staa wa soka wa Nigeria atakayekuja Tanzania mwezi Septemba....

Picha
Kiungo wa kimataifa wa  Nigeria  anayeichezea klabu ya  Chelsea  ya Uingereza  John Obi Mikel   ambae pia anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji matajiri zaidi  Africa  na katika historia ya  Nigeria ,  Obi Mikel   amecheza klabu ya  Chelsea  kwa miaka mingi amefanikiwa kuchuma fedha nyingi lakini pia ana miliki nyumba ya kifahari Uingereza na magari ya kifahari. Miongoni mwa magari anayomiliki ni  Bentley Continental GT ,  Mercedes G Wagon ,  Black Mercedes G 500  na  Range Rover Sport .  John Obi Mikel   huenda atakuja Tanzania  mwezi Septemba na timu yake ya taifa ya  Nigeria  kwani itacheza mchezo wa kuwania kufuzu katika michuano ya  AFCON 2017  na timu ya taifa ya  Tanzania, Taifa Stars. SOURCE:Millardayo.com

Sitaki mchezo, asema Lowassa...

Picha
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowasa akiwapungia mkono wafuasi wa chama hicho baada ya kuwasili katika viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya jana.  Mbeya.  Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na Ukawa, Edward Lowassa jana alipokewa na maelfu ya watu mjini hapa ambao kwenye uwanja wa Ruanda, Nzovwe, aliwaambia wananchi kuwa hatataka mchezo katika serikali atakayoiongoza. Pamoja na Jeshi la Polisi kutangaza kuzuia msafara wakati wa ziara ya waziri huyo mkuu wa zamani, hali ilikuwa tofauti jana wakati zaidi ya magari 20 yalimsindikiza kutoka Uwanja wa Ndege wa Songwe huku wananchi wakijitokeza barabarani kumshangilia hadi kwenye uwanja huo, ulio nje kidogo ya mji wa Mbeya ambako alihutubia. Polisi walinda msafara Msafara wa Lowassa uliwasili mjini hapa kwa kutumia ndege mbili, ya kwanza ikiwa imebeba waandishi wa habari wapatao 10 na nyingine iliyombeba mbunge huyo wa Monduli ambayo iliwasili saa  8:20. Umati wa watu ulikuwa ukimsubiri nje ya uwanja h

Magazeti ya Leo Jumamosi Agosti 15,2015...

Picha
SOURCE:Millardayo.com

Hivi ndivyo FC Bayern Munich ilivyoanza kwa kishindo kutetea ubingwa wao...

Picha
Ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga imeanza rasmi leo kwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo FC Bayern Munich kuwakaribisha Hamburg katika dimba la Alianz Arena. Wakicheza mchezo wa kuvutia na wa kasi FC Bayern wameibuka na ushindi wa magoli 5-0. Beki wa Kimorocco Mehd Benatia alianza kuifungia Bayern goli katika dakika ya 27 ya mchezo kabla ya Robert Lewandoski kuongeza la pili katika dakika ya 53.  Mshambuliaji wa kijerumani Thomas Muller alifunga mara mbili ndani ya dakika 4 za mchezo huo katika kipindi cha pili dakika ya 69 na 72.  Kiungo mpya wa timu hiyo Douglas Costa alifunga ukurasa wa magoli matano ya Bayern kwa kufunga goli la kwisho katika dakika ya 87. Bayern wanakaa kileleni mwa Bundesliga wakiwa na pointi 3 na magoli ya kufunga 5 huku wakiwa hawajaruhusi wavu wao kuguswa. SOURCE:Millardayo.com

Hamahama ya wanasiasa yatikisa vyama..

Picha
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja akizungumza na waandishi wa habari wakati yeye na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita (wa pili kulia), wakitangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chadema.  Kulia ni Sheikh Sadick Burhani kutoka Jumuiya na Taasisi za Kiislamu na Shura ya Maimam.  Dar es Salaam.  Wimbi la wanasiasa kuhama vyama wakati wa uchaguzi limekuwa la kawaida, lakini miaka 20 baada ya siasa za vyama vingi kurejeshwa, hali hiyo inaonekana kutikisa vyama hasa baada ya kutawaliwa na mawaziri, wabunge na madiwani. Tangu Rais Jakaya Kikwete atoe hotuba yake ya mwisho kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano, wanasiasa wamekuwa wakitangaza kukimbia vyama vyao, na hali hiyo ilikolezwa baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuihama CCM na kujiunga na Chadema mwishoni mwa Julai, baada ya jina lake kuenguliwa kwenye mbio za urais za CCM. Sababu kuu ambazo zimekuwa zikitolewa wakati wanasiasa hao wanapohama ni majina yao k

Barcelona hali mbaya – hiki ndio kipigo walichopokea kutoka kwa Athletic Bilbao...

Picha
Baada ya katikati ya wiki kupata ushindi wa 5-4 dhidi ya Sevilla katika mchezo wa UEFA Supercup, klabu bingwa ya ulaya FC Barcelona leo wamekutana na kipigo kizito kutoka kwa Athletic Bilbao. Vilabu hivyo vilivyocheza fainali ya kombe la mfalme wa Hispania msimu uliopita, leo vilikutana kwenye mchezo wa Spanish Supercup ambao umemalizika kwa Barca kufungwa magoli 4-0. Kiungo San Jose alifungua akaunti ya magoli ya Bilbao katika dakika ya 14 – goli lilodumu mpaka kipindi cha kwanza kilipomalizika. Kipindi cha pili Bilbao walicharuka na kufunga magoli mengine matatu kupitia mshambuliaji hatari Aduriz, aliyefunga katika 53, 62, na dakika ya 68.  Timu hizo zitarudiana wiki mbili zijazo katika dimba la Nou Camp. SOURCE:Millardayo.com

NEMC imekifunga kiwanda cha kusindika nyama ya Punda mkoani Dodoma...

Picha
Baraza la taifa la usimamizi wa mazingira {NEMC} limekifungia kiwanda cha Huwa Cheng Company Limited kilichopo mjini Dodoma na kukitoza faini ya shilingi milioni 200 baada ya kubaini kiwanda hicho kinajihusisha na usindikaji wa nyama ya Punda kinyume na utamaduni wa watanzania huku mazingira yake yakiwa hatarishi kutokana na uchafu unaozalishwa kuzagaa kwenye makazi ya watu. Ni mabishano makali baina ya wamiliki wa kiwanda hiki raia wa uchina na maofisa wa NEMC yaliyochukua muda mrefu kabla ya maofisa hao kutoa tamko la kufungwa kwa kiwanda hicho ambacho mbali na kuzalisha nyama ya Punda ambayo ni kinyume na utamaduni wa watanzania lakini pia mazingira ya uzalishaji wake ni hatarishi kwa afya za wafanyakazi na majirani wa eneo hilo.   Kiwanda hiki ambacho kwa siku kinadaiwa kuchinja Punda wasiopungua 200 inaelezwa kuwa mbali na kukiuka utamaduni lakini pia kinaharibu kizazi cha wanyama hao ambao uzao wake unatajwa kuwa ni mdogo hali inayotishia wanyama hao ambao kwa kanda ya

RockStar4000 watangaza ujio wa Collabo kali ya Allikiba na Ne-Yo....

Picha
Kampuni inayomsimamia Alikiba, Rockstar4000 imetangaza kuwa msanii huyo atamshirikisha msanii wa Marekani, Ne-Yo. Imetoa tangazo hilo kupitia Instagram. “Exciting News: African superstar Alikiba will be collaborating with International Superstar Ne-Yo — More news to follow…. #kingkiba #ROCKSTAR4000,” imeandika. Ne-Yo ambaye alitumbuiza kwenye tuzo za MTV MAMA mwaka huu, anatarajia kuja tena Afrika hivi karibuni ambapo ataungana na wasanii waliopo kwenye kipindi cha Coke Studio Afrika jijini Nairobi, Kenya. Alikiba ni miongoni mwa wasanii waliopo kwenye msimu huo mpya. Album mpya ya Ne-Yo Non-Fiction ilifika namba moja kwenye chati ya Billboard’s Top R&B/Hip-Hop Albums. Pamoja na Ne-Yo, Alikiba pia anatarajia kumshirikisha msanii wa Nigeria, Davido. SOURCE:BONGO

Japan inajutia vita vya pili vya dunia...

Picha
Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, ameeleza kusikitishwa kwake na mateso Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, ameeleza kusikitishwa kwake na mateso na kujitolea kwa watu wengi wakati wa vita vya pili vya dunia. Katika hotuba aliyotoa kuadhimisha miaka 70 tangu kushindwa nchi yake katika vita hivyo, Abe ameeleza alichokitaja kuwa kujutia makosa yaliofanywa dhidi ya wanawake ambao walinyimwa heshima zao wakati wa vita. Amesema Japan inapaswa kuhakikisha kwamba mzozo wa aina hiyo hautokei tena. Manusura wa vita vikuu vya pili vya dunia mjini Hong Kong wameandamana wakitaka fidia Bwana Abe ameitoa kauli hiyo wakati wa sherehe za maadhimishisho ya miaka sabini tangu Japan iliposhindwa vita hivyo Wakati huo huo kundi la manusura wa vita vikuu vya pili vya dunia mjini Hong Kong wamefanya maandamano nje ya ubalozi mdogo wa Japan kudai fidia kwa kupoteza pesa ambapo wanasema walipata shida kutokana na Japan kuuvamia na kuuteka mji wao . Hotuba hiyo ilikuwa ya kuadhimisha miaka 70 t

Ubalozi wa marekani wafunguliwa Cuba...

Picha
Bendera ya Marekani imepepea tena Cuba Sherehe za ufunguzi wa ubalozi wa Marekani huko Cuba zimefanyika mjini Havana. Bendera hiyo imerejea Cuba baada ya miaka 50 Hii ndio mara ya kwanza kwa ubalozi huo na haswa bendera ya Marekani kupepea tena nchini humo tangu mwaka wa 1961. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, aliyeko Havana ndiye aliyekuwa mgeni mheshimiwa katika dhifa hiyo ya kufungua upya ubalozi wa nchi yake nchini Cuba. Ubalozi wa marekani wafunguliwa Cuba baada ya zaidi ya nusu karne ilipofungwa. Hii ndio mara ya kwanza kwa ubalozi huo na haswa bendera ya Marekani kupepea tena nchini humo tangu mwaka wa 1961. Katika sherehe zilizofanyika Havana, Kerry aliandamana na wanajeshi watatu wa zamani ambao waliishusha bendera ya Marekani katika jengo la ubalozi huo mnamo 1961. Rais Obama na mwenzake wa Cuba Raul Castro walikubaliana mnamo December mwaka jana kuurudisha uhusiano wa kidiplomasia. Rais Obama na mwenzake wa Cuba Raul Castro wali

Wahamiaji 100 kutoka Asia wanaswa Uganda...

Picha
Wahamiaji kutoka Asia waliokamatwa Urusi, wahamiaji wengine 100 wamekamatwa Uganda Polisi nchini Uganda inamshikilia mshukiwa mmoja na kumsaka mwingine katika kile kinachoonekana kama kusafirisha watu kinyume na sheria. Aidha wanajiandaa kuwarejesha makwao wahamiaji 30 kati ya 100 waliokamatwa. Kuna raia zaidi ya 100 kutoka bara hindi ambao wako mjini Kampala wakidai walihadaiwa na tapeli mmoja aliewaahidi kuwapa ajira nchini Afrika Kusini lakini mtu huyo hajulikani mahali alipo. Polisi hao wanasema huenda kukawa mtandao wa watu wanaosafirisha kimagendo watu kutoka nje ya nchi kuwaleta hapa na pia kuwapeleka kwingineko kwa visingizio vya kuwapatia ajira kinyume na utaratibu ulioko. Hii inatokana na taarifa kuwa raia zaidi ya 20 kutoka bara hindi wamekuwa katika mahote limbalimbali mjini Kampala wakisubiri kupelekwa nje Raia hao kutoka bara hindi waliingia Uganda kama watalii lakini aliewaleta akatoweka na hivyo kubaki wakichanganyikiwa bila pesa za kulipia chakula na mala