Mwenyekiti wa CCM wilayani Sumbawanga Bw Emmanuel Kilindu ajiuzulu...
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wa wilaya ya Sumbawanga mjini Bw Emmanuel Selemani Kilindu, amechukua hatua ya kujiuzulu wadhifa wake huo kufuatia kuhitilafiana kwa kiwango kikubwa na mbunge anayemaliza muhula wake, na kudai kuwa licha ya kukabiliana na changamoto nyingi za kiutendaji lakini pia anayaweka maisha yake kwenye hatari kubwa.
Akiongea na waandishi wa habari mjini Sumbawanga mbele ya baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi, mwenyekiti huyo wa CCM Bw Kilindu amesema mbunge anayemaliza muhula wake katika jimbo la Sumbawanga mjini Aeshi Hilal, amekuwa akikiuka kanuni nyingi za chama ikiwa ni pamoja na kuwatumia wapambe wake kufanya vurugu hadi kufikia kutaka kuichoma kwa moto ofisi ya chama hicho kwa maslahi yake, huku mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi ya wilaya hiyo Bw Michael Chifunda akimuunga mkono naye kwa kuachia ngazi.
Kwa upande wao baadhi ya wanachama wa CCM wakiongea kuhusu sakata hilo, wamesema chama sasa kimefikia mahali pabaya kwa watu kutumia fedha zao kuwagawa wanachama na viongozi pia na kuwa kwenye makundi, hali ambayo inaelekea kukidhoofisha chama hivi sasa.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni