Mzozo mkubwa umezuka kwa wananchi wa kijiji cha Msowero kupinga kugawanywa kwa vijiji...


Mzozo mkubwa umezuka kwa wananchi wa kijiji cha Msowero Wilayani Kilosa kufuatia uongozi wa kata Kugawa vijiji vingine bila ridhaa ya mkutano mkuu wananchi husika ambapo wametishia kuwafikisha mahakamani.

Wakizungumza kwa jaziba wananchi hao wamewalalamikia viongozi hao kufanya utapeli wa kugushi hati ya makubaliano ya kijiji na kusainisha majina ya watu waliokufa kugawa vijiji vingine ambavyo ni kijiji cha Mvumi na mkogwe ambapo wamesema maamuzi hayo sio ya wananchi husika nakuahidi kuwafikisha mahakamani.
 
Kwa upande wake aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji cha Msowero Mbaya Ngazimba amekataa vikali kuhusika na utaratibu huo wa kugushi hati ya kijiji na kutupia lawama uongozi wa watendaji kata na akiwepo aliye kuwa diwani wa kata hiyo Hassani Mkopi.
 

SOURCE:ITV

















Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..