Maamuzi walioamua Vodacom kuhusu udhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara..

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF August 12 limeingia mkataba wa udhamini na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom wa kuendelea kuidhamini Ligi Kuu Tanzania, Vodacom wamekuwa wakidhamini Ligi hiyo kwa takribani miaka nane na wameingia mkataba mpya wa miaka mitatu wakuendelea kudhamini Ligi hiyo.

DSC_1051
Mkataba huo ulisainiwa mbele ya waandishi wa habari huku kukikwa na Rais wa TFFJamal Malinzi na Afisa mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi Borniface Wambura huku upande wa Vodacom ukiwakilishwa na meneja masoko wa kampuni hiyo Kelvin Twissa.
DSC_1036
Mkataba wa sasa umeberoshwa kwa kiwango cha fedha kwani uliomalizika ulikuwa na thamani ya bilioni 1.6 huku huu wa sasa umeongezeka kwa asilimia 40 zaidi ya ule wa awali nakufanya thamani yake kuwa bilioni 2.3.
“TFF tunayo furaha kubwa sana kuweza kukaa na ndugu zetu hawa wa Vodacom katika kuhitimisha kile tulichokuwa tunakifanya kwa muda wa mwaka mzima, Mungu ametusaidia leo hii tunasaini mkataba mwingine wa miaka mitatatu utakao tupeleka kwa kipindi cha msimu huu na 2016-2017 na 2017- 2018″>>>Jamal Malinzi
“Ligi zipo zaidi ya nane ukitoa Premier League mwenye interest ya kuingia kwenye mpira aingie lakini kuniambia leo hii mimi niruhusu mwingine aingie hapana tunadhamini hii kitu ili kukuza biashara yetu na kusaidia soka”>>> Kelvin Twissa
SOURCE:Millardayo.com






Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..