BUNGE LA IRAQ LAUNGA MKONO VITA DHIDI YA UFISADI
BUNGE la Iraq limepiga kura kwa wingi kuunga mkono mapendekezo yaliotolewa na waziri mkuu Haider al Abadikwa lengo la kukabiliana na ufisadi pamoja na kupunguza matumizi ya fedha serikalini.
Spika wa bunge hilo Salim al Juburi amesema kuwa muswada huo umepitishwa bila upinzani wowote ambao unalenga kupunguzwa kwa baadhi ya nyadhfa serikalini, kumaliza ubaguzi wa kidini pamoja na wa kisisasa.
Hatua hiyo imefikiwa wakati ambapo kumekuwa na maanadamano ya raia kuhusu kukatika mara kwa mara kwa umeme wakati ambapo kuna joto jingi mbali na ufisadi serikalini unaosababishwa na uzembe.
SOURCE:Efm radio
Maoni
Chapisha Maoni