Jeshi la Polisi lasalimu amri kwa Lowassa...
Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam limefikia muafaka juu ya maandamano ya kumsindikiza mgombea urais wa CHADEMA kuanzia ofisi za CUF buguruni Dar es Salaam na kumalizia makao makuu ya Chadema.
Hapo awali Jeshi la Polisi lilipiga marufuku maandamano hayo kwa kile walichodai ni kuwa Mh.Edward Lowassa ni mgombea wa tiket ya Chadema na hivo hawayatambui maandamano yatakayoanzia ofisi za CUF.
Wakati kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam kamishna Suleiman Kova akitoa taarifa za Polisi kuzuia maandamano ya chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA hapo awali ,mwenyekiti mwenza wa UKAWA ambaye pia ni mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ameeleza kuwa hawajapata taarifa za zuio hilo kuanzia ofisi za CUF badala yake wataendelea na ratiba yao kama ilivyo pangwa.
Pia Jeshi hilo la kanda maalumu ya DSM lilikanusha kupiga marufuku maandamano hayo bali Kamanda wa polisi kanda maalum ya DSM Suleiman Kova amesema kuwa maandamano wanayo yatambua ni yanayo anzia CHADEMA kwenda NEC na kurudi Chadema makao makuu kinondoni,lakini ya kutoka Nec kwenda makao makuu ya CUF buguruni hawayatambui.
SOURCE:Mzalendo.net
Maoni
Chapisha Maoni