Wananchi wa Lemara mkoani Arusha wakumbwa na hofu ya kuathiriwa na majitaka yenye sumu...
Wananchi wa kata ya Lemara jijini Arusha wamekumbwa na hofu ya usalama wa maisha yao baada ya bwawa la majitaka lililoko katika eneo hilo kutiririsha maji yanayodhaniwa kuwa na sumu zinazotoka viwandani na wameziomba idara zianzohusika kuchukua hatua kabla madhara kutokea .
Wananchi hao wamesema wamekuwa na wasi wasi baada ya maji hayo kuanza kubadilika rangi na wanasema wanapouliza wameambiwa kuwa tatizo hilo linafanyiwa kazi ahadi ambayo haijatelekezwa.
Aidha wananchi hao wamesema mabadiliko ya rangi ya maji katika bwawa hilo pia yanahusishwa na habari zilizoenea kuwa baadhi ya magari yamekamatwa yakiwa yanamwaga majitaka ya viwandani yanayodhaniwa kuwa na sumu kwenye mifumo ya majitaka mamlaka ya maji jambo linalodaiwa kusababisha matatizo makubwa kwenye mfumo wa kusafisha majitaka.
Akizungumzia malalamiko ya wananchi hao afisa uhusiano wa mamlaka ya majisafi na majitaka jijini Arusha (AWUSA) Bw.William Shayo amekiri kuwepo kwa matatizo katika mfumo wa kusafisha maji kwenye bwawa hilo na pia kukamatwa kwa gari likimwaga maji kwenye mtandao wa (AWUSA) kinyume cha sheria.
Aidha Bw Shayo amesema mamlaka imeshachukua hatua za kukabilianana tatizo hilo ikiwemo ya kuchunguza maji hayo kama yana sumu amala na kwamba pia jitihada za kubaini kiwanda kilichohusika pia zinaendelea.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni