Pichaz:Katika jeans hii unaiweka simu yako poa kabisa, inachaji huku unaendelea na mambo mengine...





Kumegunduliwa powerbank ambazo zinaokoa sana watumiaji wa smartphone, lakini ubunifu haujaishia hapo… sasahivi zimekuja mpaka jeans, ndio…. Unavaa suruali yako fresh kabisa alafu unatundika na smartphone yako na betri yake inaendelea kuingiza chaji mdogomdogo!

Jeans yenyewe imeingizwa sokoni Marekani kwa dola 189 (Tshs. 400,000/= kwa sasa), utaweza kuchaji smartphone yako alafu kila kitu kinakuwa sawa… usihofu kwamba simu yako itaanguka, kuna sehemu poa ya kuweka simu pamoja na betri yenye chaji ili iendelee kuchaji simu yako popote ulipo.
Sehemu ya kuweka simu ni kama kimfuko hivi juu ya mfuko wa nyuma wa jeans, ila kama simu yako ni kubwa kuliko iPhone 6 basi itakuwa bahati mbaya yako, haitoweza kuingia.
Hapo unaichomeka simu yako, na Powerbank au betri ili iendelee kuingiza chaji kwa urahisi zaidi bila kujiongezea mizigo mkononi… Jeans yenyewe inaitwa #Hello Jeans, ni ubunifu wa Joe’s Jeans.

SOURCE:Bongo








Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..