Mauaji ya vikongwe kanda ya ziwa yamepungua kutoka 39 mwaka 2011 hadi kufikia mawili...
Mauaji ya wazee vikongwe kwa tuhuma za ushirikina na macho mekundu katika wilaya za kwimba na Magu mkoani wa Mwanza, yamepungua kutoka 39 mwaka 2011 hadi kufikia mawili agosti mwaka huu,huku serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na shirika la help age international,vikiihamasisha jamii kubadili fikra na mtazamo potofu wa kuamini kwamba kuwa na macho mekundu kwa mwanamke mzee kuna uhusiano wa moja kwa moja na uchawi.
Hayo yamesemwa na kaimu mkuu wa mkoa wa mwanza baraka Konisaga wakati akifungua mkutano wa kujadili masuala ya unyanyasaji na vitendo vya ukatili kwa wanawake wazee kutoka wilaya za magu, Kwimba,Karagwe na Kyerwa ambao umeandaliwa na shirika la kimataifa la HELP AGE INTERNATIONAL linalofanya kazi kwa kushirikiana na MAPERECE pamoja na shirika la kusaidia wazee karagwe( SAWAKA )katika mradi wa kulinda na kuenzi haki za wanawake wazee hapa nchini.
Meneja wa miradi ya kulinda na kuenzi haki za wanawake wazee Tanzania kutoka shirika la HELP AGE INTERNATIONAL Joseph Mbasha anasema kumekuwepo na jitihada za kuhakikisha kuwa wazee wanatimiziwa matakwa yao ya msingi likiwemo suala la usalama wa maisha yao, ingawa amekiri kuwepo kwa vitendo vya ukatili hususani kwa wanawake wazee ambavyo vinaendelea kufanyika katika jamii na kuwafanya waishi kwa hofu na wasiwasi mkubwa.
Ofisa mnadhimu wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza, kamishna msaidizi wa polisi Japhet Lusingu anaeleza sababu zilizochangia kushamiri kwa mauaji hayo ya kikatili na juhudi zinazoendelea kufanywa na jeshi la polisi, ikiwemo kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi ambavyo vinahusisha polisi jamii na sungusungu.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni