Watanzania watakiwa kuchambua na kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo..
Watanzania wametakiwa kuwachagua viongozi walio na moyo wa dhati wa kuwaletea maendeleo ya haraka kwa kutumia rasilimali za nchi zilizopo na kuachana na viongozi wanaotumia mbwembwe nyingi kujitangaza kwa kuwa nchi haihitaji viongozi wa mbwembwe bali wenye maamuzi kwa ajili ya maendeleo ya nchi kwa kuwa viongozi wenye ndimi mbili na mbwembwe za nguvu ya fedha hawafai kuwaongoza na kuwaondoa katika umasikini watanzania.
Akizungumza katika ofisi za makao makuu ya chama cha mapinduzi mkoani Mtwara kwa lengo la kuwasalimu na kuwashukuru wanaccm 231 waliojitokeza kumdhamini katika fomu iliyotolewa na tume ya taifa ya uchaguzi katka kinyang`anyiro cha kugombea urais, mgombea huyo wa chama cha mapinduzi Dr John Pombe Magufuli pamoja na mambo mengine amewaondoa hofu watanzania na wanaccm kwa ujumla kutotishika na baadhi ya watu wachache wanaohamia katka vyama vya upinzani baada ya kukosa nafasi ya kupata madaraka ndani ya CCM kwa kuwa lengo lao ni madaraka na si kuwatumikia wananchi huku akifananisha jambo hilo na mti unaopukutisha majani ili uweze kustawi vyema.
Aidha Dr Magufuli amesema matatizo ya watanzania wote wakiwemo walemavu anayafahamu na kwamba moyo wake uko tayari kuwatumikia wananchi kwa nguvu zake zote ili kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati na kwamba hayuko tayari kuhukumiwa duniani na mbinguni kwa kushindwa kuwatumikia vyema wananchi wa Tanzania.
Aliyekuwa naibu katibu mkuu wa CCM na mgombea ubunge wa jimbo Iramba Mh Mwigulu Nchemba amesema baadhi ya viongozi wa waliojiengua CCM wameondoka kwa lengo la kusaka madaraka ili kurejesha fedha wanazodaiwa kutokana na kutumia fedha nyingi katika chaguzi za ndani ya chama kutafuta uungwaji mkono baada ya kutemwa CCM kutokana na maadili yao kuwa ya mashaka.
Kufuatia hali hiyo watanzania wametakiwa kuwa makini na viongozi waliondoka CCM lakini pia kuzingatia kauli ya hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyewaonya watanzania kumwogopa kama ukoma mtu anayesaka madaraka hasa ya kwenda ikulu kwa udi na uvumba kwa kutumia nguvu ya fedha na kwamba umoja ni ushindi.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni