Hakuna chakula cha msaada kwa wavivu - Samia
Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa ziarani mkoani Mara.
Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kamwe Serikali haitagawa chakula kwa wananchi wavivu ambao hawataki kufanya kazi na kusubiri chakula kutoka Serikalini.
Ametoa kauli hiyo leo wakati akihutubia mamia ya wananchi wa Manispaa ya Musoma katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mukendo, mjini Musoma.
Samia amesisitiza kuwa Serikali itapeleka chakula kwa wananchi ambao mazao yao yaliharibiwa kwa mvua au yalikauka kwa ukame au kwa maafa mengine na siyo kwa wananchi wanaokaa vijiweni mchana kutwa bila kufanya kazi wakisubiri neema ya chakula kutoka kwa Serikali.
Amewahimiza wananchi kote nchini kuendelea kufanyakazi kwa bidii ikiwemo shughuli za kilimo na waache tabia ya kuuza mazao yote wanayovuna ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa chakula kwenye familia zao.
Makamu wa Rais pia amewataka viongozi wa Mkoa wa Mara washirikiane na wananchi katika kuwaelemisha mbinu bora za kilimo ili waweze kupata mazao mengi ikilinganishwa na hali ilivyo kwa sasa.
Source:Azam Tv
Maoni
Chapisha Maoni