Uingereza yawatahadharisha raia wake wanaokwenda Ethiopia..


Ofisi ya Jumuiya ya Madola na masuala ya kigeni ya Uingereza (FCO) imewataka raia wake wanaofanya safari nchini Ethiopia kuwa makini na suala la kuzimwa kwa intaneti.
Hivi karibuni, wakati wanafunzi wakifanya mtihani wa Taifa nchini humo, intaneti ilizimwa kwa siku 10 ili kuzuia wizi wa mitihani hiyo.
Hata hivyo tayari, Ethiopia ilisharuhusu intaneti hiyo kufanya kazi ila Uingereza inahofia huenda Serikali ya nchi hiyo ikaizima tena.
Hali hiyo inahofiwa kuwa huenda ikawapa shida raia wake katika suala la mawasiliano na hivyo ubalozi kushindwa kuwasaidia.
Tahadhari hiyo pia, imetolewa kwa baadhi ya maeneo ambayo raia hao hawapaswi kuyatembelea, ikiwemo kilomita 10 ya mipaka inayopakana na Ethiopia.
Mipaka hiyo ni pamoja na ile ya Somalia, Kenya, Eritrea, Sudan na Sudan Kusini.
Ethiopia kwa sasa iko katika hali ya tahadhari, iliyowekwa mwaka 2016, ili kuzima maandamano yanayoendelea nchini humo.


Source:Azam Tv


















































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..