Mfalme Saudi Arabia abadili uteuzi wa mrithi wake..


Mfalme wa Saudi Arabia amemteua kama mrithi mtoto wake Mohammed bin Salman badala ya mpwa wake, Mohammed bin Nayef aliyetangazwa awali.
King Salman pia ameagiza  Mwana mfalme Mohammed bin Salman, 31, kuwa Naibu waziri mkuu wakati akiendelea na uwaziri wa ulinzi.
Mwana mfalme Mohammed bin Nayef, mwenye  57, pia ameondolewa katika nafasi yake ya Ukuu wa masuala ya usalama wa ndani, kimesema chombo cha habari cha taifa.
Ameapa kuwa mwaminifu kwa mteule huyo mpya wa Kifalme, Shirika la habari la SPA limeripoti.
Mfalme Salman, 81, alichukua nafasi hiyo Januari 2015 baada ya kifo cha kaka yake Abdullah bin Abdul Aziz.
Alitangaza mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri miezi michache baadaye, pia alimteua mwanamfalme Mohammed bin Nayef  kama mrithi wake na Mohammed bin Salman kama naibu.
Wachambuzi walielezea mabadiliko hayo kama kuvunjwa kwa utamaduni  wa utawala wa awali wa kiongozi wa Saudi Arabia wa miaka yao ya 70 au 80.
Katika tangazo lake la hivi karibu la Mwanamfalme  Mohammed bin Salman, mwenye matamshi ya haraka  yanaonyesha kuwa kijana huyo  wa kisasa ni ishara ya mambo kubadilika.
Akiwa waziri wa ulinzi na naibu mrithi wa mfalme, aliweza kuongoza vita dhidi ya Yemen, sanjari na kuweza kusimamia vyema sera za nishati nchini humo.
Mwanamfalme aliyepokwa nafasi hiyo Mohammed bin Nayef anasifiwa kwa kuwa kiongozi wa masuala ya usalama wa ufalme huo kwa muda mrefu na kwamba ni mwenye uhusiano mzuri na washiriki wao nchi za magharibi hususani Marekani na Uingereza.


Source:AzamTv

















































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..