Utafiti uchaguzi Kenya: Uhuru kuongozi duru ya kwanza..

Picha za wagombea urais wa vyama vikuu vya upinzani Uhuru Kenyatta na Raila Odinga


Zikiwa zimesalia siku 60 ambazo zinasubiriwa kwa hamu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Agosti 8, 2017, Vyama vyenye upinzani mkubwa, yaani Chama cha Jubilee kinachotawala na kile cha upinzania cha National Super Alliance (NASA) vimezidisha ari kwa kila upande ukitafuta kura za kuwaunga mkono.
Rais Uhuru Kenyatta wa Chama cha Jubilee amepiga kambi katika kaunta za Kisii, Nyamira na Uasin Gishu  wakati wapinzani wake NASA chini ya kiongozi wao Raila Odinga, wameelekea pande za Pwani na mikoa ya Ukamban kwaajili ya kujihami.
Makundi hayo makuu mawili yamekuwa na kazi moja tu yakuwahamasisha wafuasi wao kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura katika Uchaguzi wa Agosti, na wachambuzi wa masuala ya uchaguzi wanabashiri kuwa, uchaguzi utakuwa wenye upinzani wa hali ya juu katika historia ya Kenya.

 Katika Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na kundi la uangalizi wa Uchaguzi Afrika, umeonyeshaa kuwa katika wapigakura waliojiandikisha ni asilimia 89 tu ndiyo watakaopiga kura siku hiyo ya Agosti 8. Hii ikimaanisha wapiga kura milioni 16 ndiyo watakaopiga kura kati ya milioni 19.2 ya waliojiandikisha.

Katika utafiti huo, umeonyesha kuwa Rais Uhuru Kenyatta ataibuka mshindi katika duru ya kwanza kwa asilimia 51.7 dhidi ya mpinzani wake Odinga anayedaiwa kuibuka na asilimia 39.
Mwaka 2013, Rais Kenyatta aliweza kumshinda Odinga kwa zaidi ya kura 800,000 baada ya kujinyakulia kura 6,173,433 sawa na asilimia  (50.51%) dhidi ya Odinga 5,340,546  sawa na asilimia 43.7, kati ya watu milioni 12.3 waliojiandikisha ikilingana na asilimia 86..
Utafiti huo umeonyesha kuwa maeneo ambayo Jubilee wanawafuasi wengi, namba ya watakaojitokeza kupiga kura itakuwa juu ukilinganisha na maeneo ya wapinzani wao NASA.





Source:Azam Tv


























































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..