Man United yainyanyasa Real kwenye mkwanja..

Licha ya kutoshiriki michuano ya Mabingwa barani Ulaya kwa kwa mafanikio kwa kipindi kirefu, Man United imewapiku mabingwa wa Ulaya, Real Madrid kwa kuwa timu yenye thamani zaidi duniani kwa mujibu wa jarida la Forbes la nchini Marekani.
Kilichoelezwa kuibeba klabu hiyo ni kuwa na chapa (Brand) yenye nguvu zaidi, pamoja na mikakati mikubwa ya udhamini na masoko iliyomo ndani ya klabu hiyo, ambayo imeiwezesha kukaa kileleni mwa orodha ya timu tajiri duniani kwa mara ya kwanza ndani ya miaka mitano ikiwa na thamani ya dola za Marekani bilioni 3.69 (zaidi ya shilingi trilioni 7 za kitanzania).
Kwa mujibu wa Forbes, Man United iliingiza mapato kiasi cha dola za Marekani milioni 765 katika msimu wa 2015/16 ikiwapiku Barcelona na Real Madrid kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 77.
Pia, utafiti wa Forbes umebaini kuwa Man United ndiyo klabu inayoingiza faida zaidi duniani ikiwa na mapato ya kujiendeshea ya dola za Marekani milioni 288 na kuizidi Real Madrid kwa dola za Marekani 107.
Katika orodha hiyo mpya ya mwaka 2017, Barcelona wamekamata nafasi ya pili ikiwa na thamani ya dola za Marekani bilioni 3.64, huku Real Madrid ambao wamekuwa vinara kwa miaka minne mfululizo, wakiporomoka hadi nafasi ya 3 wakiwa na thaman ya  dola za Marekani bilioni 3.58.
Nafasi ya nne imekwenda kwa Bayern Munich (dola bilioni 2.71)  nafasi ya tano ni Manchester City (dola bilioni 2.08), Arsenal ni ya sita ikiwa na thamani ya  dola za Marekani  bilioni 1.93, Chelsea ya saba (dola bilioni 1.85) na Liverpool ni ya nane (dola bilioni 1.26).




Source:Azam Tv



















































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..