Magunia 1,639 ya Mahindi yakamatwa Kilimanjaro...
Miongoni mwa Shehena zinazokamatwa mara kwa mara mkoani Kilimanjaro
Magunia Zaidi ya 1, 639 ya mahindi sawa tani 163.9 yamekamatwa katika eneo la West Kilimanjaro, Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro yakiwa njiani kutoroshwa kwa njia ya magendo na wafanyabiashara kwenda nchi za Kenya, Ethiopia, Somalia na Sudani ya Kusini ambazo zinakabiliwa tatizo la njaa.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema wafanyabiashara na madereva wa malori yaliyobeba shehena hiyo wataendelea kushikiliwa kwa zaidi ya saa 48 wakisubiri hatua za kiuchunguzi kukamilika, kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi za kisheria.
Hata hivyo amebainisha kuwa, awali madereva wa magari hayo walisema uongo kwamba wanapeleka mahindi hayo maeneo ya Tarekea wakati ukweli ni kwamba wanapeleka nje ya nchi, na hivyo kuamua kuzuia shehena hiyo.
Mkuu wa Mkoa huyo amesema uuzaji wa mahindi nje ya nchi ni kosa kwa sababu ni hasara na kuwashauri wanaotaka kuuza nje ya nchi wauze unga ili waweze kupata faida.
Source:Azamtv
Maoni
Chapisha Maoni