Qatar yasema masharti 13 iliyopewa hayana uhalisia..
Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Mohammed bin Abdulrahaman Al Thani, ameipinga orodha ya masharti 13, yaliyowekwa na mataifa manne ya kiarabu na kusema kuwa masharti hayo hayana msingi na wala hayana athari.
Nchi ya Qatar inakabiliwa na vikwazo vikali kutoka kwa Saudi Arabia na washirika wake ikiwemo Misri, Muungano wa Falme za kiarabu na Bahrain, wakiituhumu nchi hiyo kusaidia ugaidi.
Miongoni mwa masharti hayo, ni kukifungia kituo cha matangazo ya televisheni cha Aljazeera, ambacho kinafadhiliwa na serikali ya Qatar
Aljazeera yenyewe imeyatuhumu mataifa hayo kwamba yanataka kunyamazisha uhuru wa kujieleza
Qatar imeangukia kwenye vikwazo vya kiuchumi na kidiplomasia ambavyo havijawahi kulikumba taifa hilo hapo awali, huku Iran na Uturuki zikizidi kuisambazia nchi hiyo chakula na bidhaa zingine
Source:AzamTv
Maoni
Chapisha Maoni