Eid yaondoka na watoto mapacha Ziwa Victoria

Ziwa Victoria ambalo limesababisha vifo vya watoto wawili huko mkoani Kagera


Sikukuu ya Eid el-fitri imeacha majonzi makubwa mkoani Kagera, baada ya familia ya askari wa Kikosi cha Usalama barabarani, Hamis Kachwamba kupoteza watoto mapacha waliofariki dunia baada ya kuzama Ziwa Victoria, mkoani Kagera.
Mapacha hao Hassan na Hussein, waliokuwa na umri wa miaka 12,  walikumbwa na mkasa huo saa 11: 25 jana jioni, walipokuwa wakiogelea katika ufukwe wa Ziwa Victoria ikiwa ni sehemu ya kusheherekea  za sikukuu ya Eid.
Akizungumza na mwandishi wa Azam TV, Junior Mwemezi wa mkoani Kagera, Kamanda wa Jeshi la Polisi, Augustine Olomi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo ameliita kuwa ni la kusikitisha.
“Kuna tukio moja la watoto wawili wa familia moja walifariki jana baada ya kuzama ndani ya Ziwa Victoria, wakawa wamekufa maji.” alisema Kamanda Olomi
Baba mzazi wa watoto hao Hamis Kachwamba, ambaye amezungumza kwa majonzi, amesema alikuwa njiani wakati tukio hilo linatokea na ndipo alipoanza kupokea simu kutoka ofisini zikimtaka aende hospitali ya serikali.
“Baada ya kufika pale government (hospitali ya serikali) nikaingia kwenye chumba walichokuwa wamepokelewa na mganga akanipokea, basi akanifungulia watoto wangu nikawatambua mapacha, Hassan na Hussein,” alisema baba wa watoto hao.




Source:Azamtv

























































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..