Acacia wakubali kulipa fedha...
Rais John Magufuli alipokutana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thorntona NA kulia
Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining limited, Profesa John Thornton amesema kampuni yake imekubali kulipa fedha zilizopotea kutokana na kufanya shughuli zake hapa nchini.
Hayo yamejiri katika kikao kilichofanyika baina ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli na mwenyekiti huyo leo Jumatano, Ikulu Dar es Salaam.
Pia kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, inasema mwenyekiti huyo amekubali kujenga mtambo wa kuchenjulia dhahabu (smelter) hapa nchini.
Ujenzi ambao utafanywa kwa kushirikiana na Tanzania.
Pia Rais Magufuli amesema kuwa ataunda jopo la wataalamu watakaofanya majadiliano na Kampuni ya Barrick ili kufikia makubaliano ya kulipwa fedha hizo.
Katika ripoti iliyotolewa Jumatatu hii na Kamati ya pili iliyoundwa kuchunguza suala la makinikia upande wa kisheria na kiuchumi, iliyoongozwa na Profesa Nehemiah Osoro, Acacia ilishutumiwa kukwepa kodi, ikiwemo kufanya shughuli zake bila kusajiliwa hapa nchi.
Sourc:Azamtv
Maoni
Chapisha Maoni