Samia aagiza mawaziri wawili kufika Mara haraka

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiagana na baadhi ya wakazi wa Bunda


Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaagiza mawaziri wawili wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu kwenda mkoani Mara haraka iwezekanavyo kwa ajili ya kutatua changamoto zinazokabili sekta ya afya na migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ni kero kubwa kwa wananchi hao.
Samia ametoa agizo hilo kijijini Butiama kwa viongozi wa mkoa wa Mara katika majumuisho  ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani humo.
Ameeleza kuwa katika ziara yake mkoani Mara wananchi wamelalamikia mno kuwepo kwa  migogoro ya ardhi kati  ya kijiji na kijiji na kusuasua kwa utoaji wa  huduma za afya kutokana na baadhi ya hospitali kukosa fedha kutoka Serikalini jambo ambalo litapatiwa ufumbuzi na Waziri husika pindi watakapotembea maeneo hayo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dkt Charles Mlingwa amemshukuru Makamu wa Rais kwa ziara hiyo ya kikazi mkoani humo na amemuahidi kuwa maelekezo na maagizo aliyoyatoa yeye pamoja na watendaji wa wilaya zote za mkoa wa Mara watayatekeleza kwa uhakika.
Katika ziara yake Makamu wa Rais ametembelea wilaya za Butiama, Musoma Mjini, Tarime na kukagua, kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali  pamoja na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara.


Source:Azam Tv


























































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..