Kizimbani kwa kunajisi watoto wake..

Mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Japhet Legimani (38), amepanda kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha kujibu tuhuma za kunajisi watoto wake wa darasa la sita na kidato cha kwanza.
Akisoma hati ya mashtaka mahakamani hapo, mbele ya Hakimu Patricia Kisinda, Wakili wa Serikali, Riziki Maayu amedai mshtakiwa huyo anashtakiwa kwa kufanya kosa hilo kwa watoto wake  hao wawili  kwa tarehe tofauti tangu mwaka jana hadi Mei mwaka huu huko eneo la Daraja Mbili nyumbani kwake.
Kosa la pili  mshtakiwa anadaiwa kumnajisi mtoto wake wa darasa la sita katika vipindi vya Januari hadi Mei mwaka huu nyumbani kwake katika eneo la Salali  Daraja Mbili.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo Hakimu Kisinda alitoa masharti ya dhamana kwa mshitakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao ni waajiriwa wa taasisi inayotambulika na Mahakama na dhamana hiyo iwe ya thamani ya shilingi milioni tano.
 Hakimu Kisinda pia amempiga marufuku mshtakiwa huyo kusafiri nje ya Mkoa wa Arusha.
Mshtakiwa amekosa dhamana na amerudishwa rumande.

Source:Azam Tv













































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..