Mtoto wa Gaddafi aachiwa huru Libya....
Saif-al-Islam, mtoto wa aliyekuwa Kiongozi wa Libya Muammar Gaddaf
Saif al-Islam Gaddafi mtoto wa pili wa aliyekuwa Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi ameachiwa huru baada ya kuwa kizuizini kwa miaka sita.
Hatua ya kuachiwa kwake huru imehofiwa kuwa inaweza kutikisa zaidi hali ya kiusalama nchini Libya.
Saif al-Islam ndiye aliyependelewa na babake kuwa mrithi wake na amekuwa akizuiliwa na kundi la wanamgambo katika mji wa Zintan.
Wanamgambo wa Abu Bakr al-Siddiq Battalion walisema walimuachia huru Ijumaa lakini bado hajaoneshwa hadharani.
Mwanasheria wake, Khaled al-Zaidi amesema ameshaachiwa huru lakini hawezi kusema ni mji gani Saif al-Islam amekwenda kutokana na sababu za kiusalama.
Taarifa nchini Libya zinasema Saif al-Islam Gaddafi kwa sasa yupo na ndugu zake katika mji wa Bayda, Mashariki mwa Libya.
Source:Azam Tv
Maoni
Chapisha Maoni