Mlipuko shule ya chekechea China, Saba wafariki dunia..
wazazi katika shule ya chekechea China.
Watu saba wanadaiwa kupoteza maisha na wengine takribani 66 wamejeruhiwa katika mlipuko uliotokea kwenye shule ya chekechea nchini China, kwa mujibu wa ripoti.
Chombo cha habari cha Serikali cha Xinhua kimesema mlipuko huo umetokea jirani na shule ya chekechea ya Fengxian katika Jimbo la mashariki mwa nchi hiyo.
Polisi wa eneo hilo wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo, wamelieleza Shirika la habari la AFP na kusema uchunguzi umeanza.
Picha ambazo hazijathibitika zimeonekana kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha makundi ya watu wakiwa chini, wakiwemo watoto waliojeruhiwa. Inadaiwa mlipuko huo ulitokea wakati wazazi wamefika kuchukua watoto wao.
Hili ni tukio la pili kutokea kwa shule za chekechea kwa wiki za hivi karibuni.
Miezi kumi na 11 iliyopita, watoto kadhaa walifariki dunia baada ya kuungua moto wakiwa wamejazana katika basi wakitokea shuleni wakipita katika handaki katika jimbo la mashariki la Shandong.
Baadaye ilikuja kubainika kuwa moto huo uliwashwa makusudi na dereva, ambaye naye alifariki dunia.
Maoni
Chapisha Maoni