Mahakama ya Afrika yaitaka Tanzania kuhakikisha watuhumiwa wa makosa ya jinai wanapewa msaada wa kisheria...
Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu imetupilia mbali pingamizi la serikali ya Tanzania la kuwazuia watuhumiwa kumi raia wa Kenya wanaotuhumiwa kwa mauaji ya kutumia silaha kufikisha shauri lao kwenye mahakama hiyo imetaka watuhumiwa hao wapatiwe wanasheria wa kuwasaidia katika kesi inayowakabili ili haki zao msingi ziweze kuzingatiwa.
Akisoma hukumu ya shauri hilo jaji wa mahakama hiyo Bw.Fatsach Orguergouz amesema kwa kuwa mahakama imethibitisha kuwepo kwa ukiukwaji wa haki za watuhumiwa zimekiukwa amesema walalamikaji wanahaki ya kudai fidia na kama watahitaji wawasilishe madai yao mahakamani hapo ndani ya siku 30.
Akizungumza baada ya hukumu hiyo Bi.Evelin Chijarira kutoka chama cha wanasheria wa Afrika (PALU ) wanaowatetea watuhumiwa hao na baadhi ya wanasheria wamesema ukiukwaji haki za binadamu wakati wa kukamata na kushughulikia mashauri ya watuhumiwa bado ni mkubwa.
Raia hao wa Kenya walitiwa hatiani na Mahakama kuu ya Tanzania kwa kosa la mauaji na ujambazi wa kutumia silaha lililofanyika katika benki ya NMB tawi la Moshi mwezi may,2004.wako rumande kwa zaidi ya miaka kumi sasa kwa madai kwamba uchunguzi bado haujakamilika jambo linaloelezwa na wanasheria kuwa linaleta athari kubwa kwa watuhumiwa, kwa jamii na taifa kwaujumla.
Katika malalamiko yao watuhumiwa hao wanadai kuwa januari 2006, walikamatwa nchini Msumbiji na kusafirishwa kwa ndege ya kijeshi na kufunguliwa mashtaka ya mauaji na mashtaka 3 ya wizi wa kutumia silaha jambo wanalodai kuwa ni kinyume cha haki za binadam na madai yao ya msingi wanataka walipwe fidia na pia wapatiwe wanasheria kwani haki zao zinaendeleakukiukwa ikiwemo ya kuchelewa kusikilizwa kwa shauri lao
Hivi karibuni rais wa Tanzania Mh.John Magufuli alikaririwa akiwataka watendaji wa serikali kuharakisha utoaji wa maamuzi na pia kutenda haki.
Source:ITV
Maoni
Chapisha Maoni