Umoja wa mataifa yatoa ripoti kuhusu Sudan Kusini..
Mwanajeshi wa serikali akiwa kwenye gai la kijeshi lenye silahaya kwenye mji wenye utajiri wa mafuta wa Malakal, Sudan kusini.
Kamisheni ya haki za binadamnu ya Umoja wa Mataifa inasema serikali ya Sudan Kusini imeongoza sera ya uharibifu ya kuwauwa, kuwabaka, na kuwaibia raia ilipokua inapambana na waasi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Ripoti mpya iliyotolewa leo Ijumaa inasema pande zote katika mzozo huo zimetenda ukatili kwa mpangilio dhidi ya raia lakini anasema wale waliokuwa serikalini ndio wanawajibika zaidi wakati wa kipindi cha 2015 wakati majeshi ya upinzani yalipo dhoifika.
Ripoti hiyo inaeleza mambo kadhaa ya ukiukaji wa haki za binadamu. Ukubwa wa ghasia za ngonoi unashtusha zaidi ofisi ya haki za binadamu ilieleza katika taarifa yake. Kati ya april hadi septemba 2017 takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kulikuwepo na zaidi ya watu 1 300 walobakwa.
Source:VOA
Maoni
Chapisha Maoni