TTCL KUPUNGUZA WAFANYAKAZI 400...

Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ipo kwenye maandalizi ya kupunguza wafanyakazi wasiohitajika kwa sasa kutokana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

TTCL inayotoa huduma za simu na pia kutoa mitandao kwa kampuni zilizo na leseni ya huduma hizo, itapunguza wafanyakazi 400 ili kuongeza ufanisi na hivyo kumudu ushindani katika sekta ya mawasiliano dhidi ya kampuni binafsi. 

Mapema mwaka jana, Serikali iliamua kununua asilimia 35 ya hisa za TTCL zinazoshikiliwa na kampuni kubwa ya huduma za simu nchini India, Bharti Airtel na baadaye mwezi Mei, 2015 aliyekuwa Naibu Waziri wa Sayansi na Mawasiliano, January Makamba aliliambia Bunge kuwa Serikali iko katika maandalizi ya mwisho ya kumiliki hisa zote za kampuni hiyo kubwa kwa huduma za simu za mezani nchini.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya kampuni hiyo kinaeleza kuwa kati ya wafanyakazi 1,500 wa TTCL, zaidi ya 400 watapoteza ajira katika mpango huo wa kudhibiti gharama za uendeshaji.

“TTCL itaomba fedha ili kuwalipa wafanyakazi zaidi ya 400 wanaotakiwa kupunguzwa,” alisema mtoaji habari huyo .

“Kuna wafanyakazi wanaingia asubuhi na kutoka jioni bila kufanya kazi yoyote ile na mwisho wa mwezi anakula mshahara zaidi ya Sh800,000. Kumuachisha kazi inakuwa vigumu sana, lakini kama TTCL itasaidiwa na Serikali kufanikisha hilo, itakuwa imejikwamua kwa kiwango fulani.”

Hata hivyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura alisema maandalizi ya kupunguza wafanyakazi yataanza mwezi April kupitia ukaguzi maalumu wa rasilimali watu.






Source:Mtembezi.com













































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..