Polisi inawashikilia watu 30 wakiwamo raia 4 wa Burundi kwa mauaji Kasulu.
Watu thelathini wakiwemo raia wane wa Burundi wanashikiliwa na jeshi la Polisi wakituhumiwa kwa mauaji ya maafisa wawili wa serikali waliouawa kwa kupigwa na fimbo katika wilaya ya Kasulu mkoa wa Kigoma kufuatia mapigano kati ya wafugaji na maafisa wa wakala wa misitu tfs na askari mgambo baada ya kukamata zaidi ya ng’ombe elfu moja na mia nne.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Ferdinand Mtui amesema oparesheni ya kukamata wahusika wa tukio hilo inaendelea na watu zaidi wanatarajiwa kukamatwa na kwamba watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.
Kwa upande wao wafugaji wamesema uvunjifu wa sharia unaofanywa na maafisa kutoka wakala wa misitu ndio unaosababisha kuwepo kwa vurugu za mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji na serikali, ambapo wameiomba serikali na hasa waziri wa kilimo,chakula na ushirika kuyapatia ufumbuzi matatizo yao.
Askari mgambo Rocke Bilamuka na mwanafunzi wa chuo cha maliasili Pasiansi mkoani Mwanza Idelfonce Alfonce waliuawa katikati ya wiki hii baada ya kutokea mapigano kati yao na wafugaji katika kijiji cha mvugwe wilayani Kasulu.
Source:ITV
Maoni
Chapisha Maoni