Karatasi za kupigia kura zawasili Zanzibar..
Picha ya vijana wakiimba na kuunga mkono upinzania katika uchaguzi wa urais Zanzibar mwaka 2015.
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Ijumaa imepokea shehena ya karatasi zitakazotumika kwa ajili ya kupigia kura katika uchaguzi mkuu wa marudio unaotarajiwa kufanyika Machi 20 mwaka huu, huku ikiahidi kuwa maandalizi yote ya uchaguzi huo yamekamilika na utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.5.
Mkurugenzi huyo amesema kazi ya kusambaza karatasi hizo katika ofisi za tume za wilaya inatarajiwa kufanyika kuanzia Machi 18, na siku itakayofuata karatasi hizo zitasambazwa katika vituo vya kupigia kura vilivyopo katika visiwa vya Unguja na Pemba ikiwa ni siku moja kabla ya tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi huo.
Uchaguzi huo wa marudio unafanyika Machi 20, huku baadhi ya vyama vya siasa vikiwa vimetangaza msimamo wa kutoshiriki kutokana na sababu mbalimbali, lakini tume hiyo ya uchaguzi imechapisha picha za wagombea wote walioshiriki katika uchaguzi wa oktoba 25 ambao matokeo yake yalifutwa na Mwenyekiti wa ZEC Alhaj Jecha Salim Jecha.
Source:VOA
Maoni
Chapisha Maoni