Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi Kahama imeendelea kunguruma.
Hatimaye kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu jimbo la Kahama mjini uliofanyika tarehe 25 mwezi wa kumi mwaka jana iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema Bw.James Lembeli dhidi ya mgombea ubunge wa CCM Bw.Jumanne Kishimba imeingia hatua nyingine baada ya mahakama ya wilaya ya Shinyanga kuanza kusikiliza mashahidi wa upande wa mlalamikaji.
Kesi hiyo inayoendeshwa na jaji Moses Mzuna kutoka mahakama kuu ya Shinyanga imeendelea kusikilizwa ambapo shahidi namba moja wa upande wa mlalamikaji ambaye ni mlalamikaji mmwenyewe Bw.James Lembeli ametoa ushahidi wake mbele ya mahakama na kukabidhi vielelezo vya ushahidi kama viashiria vya rushwa kutumika katika uichaguzi huo ambapo wakili wa upande wa mlalamikiwa ameweka pingamizi katika vielelezo hivyo ambavyo ni madaftari na viberiti vilikuwa vikigawiwa watu wakati wa kampeni ambapo mahakama ilimekubali pingamizi hilo na kumtaka.
Aidha wakati akiendelea kutoa ushahidi mbele ya jaji Moses Mzuna Bw.Lembeli amesema katika kitabu cha sheria ya uchaguzi wa rais,wabunge na madiwani sehemu ya 3 kifungu cha 3 mbili sheria imekataza vyombo vya dola kutumia nguvu katika shughuli za uichaguzi lakini kinyume na hapo polisi walitumika kukamata watu na kutishia wapiga kura huku akidai kuwa matukio hayo yalifanyika siku za mwishoni hali ambayo imesababisha kura zake kuhujumiwa.
Kwa upande mwingine Bw.Lembeli ameiomba mahakama kutenda haki kwa mujibu wa sheria kutokana na ushahidi alioutoa kwakuwa uchaguzi uliopita haukufanyika kwa uhuru na haki na baada ya kesi kuahirishwa na kupangwa kuendelea siku unayofuata nje ya mahakama wananchi walitaka kujua nini m,awazo yake baada ya kutoa ushahidi ambapo aliwatuliza na kuwaomba waendelee kufuatilia mwenendo wa kesi.
Source:ITV
Maoni
Chapisha Maoni