TAARIFA RASMI YA RAIS MAGUFULI KATIKA ZIARA YA KUSHTUKIZA BENKI KUU LEO..

Rais Magufuli
Rais Magufuli akikagua CV za wafanyakazi wa Benki Kuu.
Rais Magufuli
Rais Magufuli akizungumza na ungozi wa juu wa Benki Kuu ya Tanzania.

Leo March 10 2016 Rais John Pombe Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT), ambapo pamoja na mambo mengine ameiagiza Benki hiyo kusitisha mara moja ulipaji wa malimbikizo ya malipo ambayo tayari yalishaidhinishwa (Ex-Checker) na badala yake yarejeshwe Wizara ya fedha na Mipango kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki.

Taarifa za awali zinaonyesha kuwa Benki Kuu ya Tanzania ilikuwa katika mchakato wa kufanya malipo ya shilingi Bilioni 925.6, ambazo Wizara ya Fedha ilitoa idhini ya kufanyika malipo.

Pia Rais Magufuli ameagiza Wizara ya Fedha ifanye upya uhakiki wa malipo hayo, ili kubaini kama walengwa walioidhinishwa kulipwa wanastahili kulipwa ama vinginevyo.

Na mwisho amemuagiza Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Beno Ndulu kupitia upya orodha ya wafanyakazi wa Benki hiyo, na kuwaondoa mara moja wale wote ambao hawana ulazima wa kuwa wafanyakazi katika benki hiyo.






Source:Lindiyetu.com










































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..