Chadema yasikitishwa na sarakasi za umeya wa jiji la Dar es Salaam zinazoendelea.


Uongozi wa juu wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA umeelezea masikitiko yake juu ya kile kinachoendelea kuhusu mivutano ya ni lini uchaguzi huru na wa haki wa kumpata meya wa jiji la Dar es Salaam utafanyika huku ukisema unajipanga kimkakati kuona namna ya kumpata meya huyo.

Masikitiko hayo yamo kwenye maazimio kadhaa ya kamati kuu ya chama hicho iliyokuwa ikijadili hali ya mwenendo wa kisiasa nchini baada ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na hali ilivyo kuelekea mach 20 kule visiwani Zanzibar,huku ikikosoa hali ya utawala bora nchini kwa sasa. 
 
Kuhusu hali ya mambo inavyoendelea ya kumpata Meya wa jiji la Dar es Salaam amesema hawata kuwa tayari kuona wakipigwa danadana na chama tawala kwani ni dhahili akidi wameishilikia wao.
 
Katika hatua nyingine ya kuzidi kujimarisha kwa chama hicho cha upinzania nchini, kamati kuu pia imeadhimia kuufanya mkoa wa Dar es Salaam kuwa wa kimkakati zaidi kwa kuupa jina la Dar es Salaam kuu baada ya kifungu namba 6 na 7 cha katiba ya chama hicho kuipa nguvu kamati kuu kufanya hivyo huku uongozi wa kimikoa ndani ya jiji ikibaki kama ilivyo.




Source:ITV






























































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..