Waziri Mkuu Mh.Majaliwa aahidi kushughulikia ujenzi wa daraja katika mto Kagera.
Waziri mkuu Mh.Kassim Majaliwa ameahidi kushughulikia ujenzi wa daraja katika mto kagera ambalo limekuwa changamoto kubwa kwa mawasiliano ya wakazi wa wilaya ya Misenyi na Karangwe, kutokana na ukosefu wa daraja hilo kwa muda mrefu,hali inayorudisha nyuma maendeleo kwa wakazi wa pande zote mbili.
ITV imeshuhudia msafara wa waziri mkuu akingia katika kiwanda cha Kagera Sugar ambapo baadaye akizungumza pembezoni mwa mto Kagera katika wilaya ya Misenyi waziri Mkuu Mh.Majaliwa amesema serikali itashughulikia ujenzi wa daraja hilo mara moja ili kutoa fursa ya maendeleo kwa wakazi wa wilaya hizo sambamba na wawekezaji wazawa walipo katika eneo hilo.
Kabla ya waziri Mkuu kutembelea kutembelea eneo la mto linapotarajiwa kujengwa daraja,alipata nafasi ya kuzungumza na uongozi wa kiwanda cha Kagera Sugar ili kujionea namna ambavyo kiwanda hicho kinazalisha sukari ambapo pia amepongeza uongozi kwa kutoa nafasi nyingi za ajira kwa wataalam wengi kutoka ndani ya nchi tofauti na viwanda vingine.
Source:ITV
Maoni
Chapisha Maoni