Uganda: chama cha FDC chaendelea na maombi..
Kiongozi wa upinzani Uganda, Kizza Besigye.
Wiki iliyopita, chama hicho kilitangaza kuwa kila Jumanne kitakuwa na maombi katika Ofisi zake kote nchini kuliombea taifa hilo lakini pia kuendeleza shinikizo za kuachiliwa huru kwa aliyekuwa mgonbea wao Kizza Besigye anayezuiliwa nyumbani kwake.
Msemaji wa FDC Ibrahim Ssemujju amesema nchi hiyo imeendelea kuongozwa kimabavu na rais Yoweri Museveni na wanaamini maombi yatasaidia.
Kiongozi mkuu wa Upinzani Kizza Besigye aliwekwa katika kizuizi cha nyumbani baada ya uchaguzi, huku serikali ikibaini kwamba ilifanya hivyo kutokana na kauli mbovu za kiongozi huyo pamoja na nia yake ya kutaka kuchochea uhasama kwa lengo la kuhatarisha usalama wa taifa.
Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Uganda wamekua wakilaani uamuzi wa serikali wa kutomtendea haki Kizza Besigye.
Awali Kizza Besigye alibaini kwamba uchaguzi wa urais uliofanyika nchini Uganda uligubikwa na wizi wa kura, huku akikataa kukubali matokeo ya uchaguzi huo, licha ya kusahihishwa na mahakama ya Katiba.
Maafisa wa polisi wa Uganda wakipiga kambi mbele ya nyumba ya mpinzani mkuu Kizza Besigye Februari 22, 2016, katika kitongoji cha mji wa Kampala.
Source:rFi Kiswahili
Maoni
Chapisha Maoni