Wafugaji Bariadi wakaidi agizo la waziri mkuu..


Siku chache baada ya waziri mkuu Kassim Majaliwa kuwataka wafugaji wanaoishi kandokando ya hifadhi ya Serengeti kuacha kuingiza na kuchungia mifugo yao ndani ya hifadhi hiyo,wafugaji hao ambao wengi wao ni viongozi wa kisiasa wamekaidi agizo hilo.

Wakiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mwasenase kilichopo kata ya Nkororo wilayani Bariadi wafugaji hao wamesema kamwe hawataacha kuchungia Ngo’mbe wao hifadhini kwakuwa hawana sehemu nyingine ya kupeleka mifugo yao.
 
Mkuu wa wilaya ya Bariadi Ponsiano Nyami amewataka wafugaji hao kuacha kuingiza mifugo yao hifadhini na kufuata sheria kwani iwapo watapuuza wataendelea kukamatwa na askari wa hifadhi hiyo ambao wako kisheria na wanatimiza wajibu wao na kwamba sheria hiyo imetungwa na bunge hivyo wasikubali kudanganywa na wanasiasa ambao wamekuwa wakitafuta kura kwa kuwadanganya kuwa wakiwachagua watachungia hifadhini.
 
Kwa upande wake mkuu wa hifadhi ya Serengeti William Mwakilema amewataka wananchi waishio kando kando ya hifadhi hiyo kupanga matumzi bora ya ardhi  huku akiwataka kuheshimu  mipaka iliyowekwa na hifadhi hiyo ambapo kila mwananchi anatakiwa kuacha mita 500.kama sheria inavyosema.
 
ITV imeshuhudia makundi makubwa ya Ngo’mbe zikiwa  zinaingizwa ndani ya hifadhi ya serengeti kwa ajili ya kuchunga huku watoto wadogo wakiachiwa kuchunga mifugo hiyo ndani ya hifadhi.





Source:ITV


















































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..