HII NI NAFASI YA MWISHO KWA ZLATAN IBRAHIMOVIC KUCHUKUA NDOO YA UEFA..


Kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita hakuna mchezaji aliyepata mafanikio makubwa katika ngazi ya Ligi ya ndani zaidi ya Zlatan Ibrahimovic. Msimu huu anajiandaa kuchukua Kombe la Ligi kuu Ufaransa akiwa na klabu yake ya Paris Saint Germain inayoongoza ligi hiyo kwa tofauti ya pointi 23 na kuna uwezekano wa yeye kumaliza mfungaji bora wa ligi hiyo kutokana na kuwa na magoli 20 mpaka sasa.
Hii ina maana kwamba atakuwa ameshinda makombe 9 ya Ligi mbalimbali pamoja na tuzo 5 za mfungaji bora kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita.
Licha ya kupata mafainikio hayo lakini maisha ya soka kwa mwanandinga huyo kutoka Sweden yamegubikwa na utata kutokana na watu kusema kuwa yeye ndiye aliyeifanya Barcelona kuwa mbaya katika kipindi cha mwaka mmoja aliokaa Nou Camp, na wengine wanadai Ligue 1 siyo ligi yenye ushindani kiivyo.
Lakini doa kubwa katika mafanikio yote hayo ya Zlatan ni kukosa ndoo ya Uefa, Ibrahimovic hajawahi kushinda kombe la UEFA na ni wazi hajawahi kufanikiwa hata kukaribia kubeba na akiwa anaelekea kutimiza miaka 35 huu unaweza kuwa msimu wake wa mwisho kufanya hivyo.
Tangu mwaka 2006 amefika hatua ya 16 bora mara nne na hatua ya robo fainali mara nne lakini amefanikiwa kufika nusu fainali mara moja tu katika msimu wake mmoja na Barcelona. Hadhi yake pia katika soka la Ulaya imeshuka kutokana na kuondolewa kwenye mashindano na timu zake za zamani mara nne ndani ya msimu sita.
Lakini kwanini hasa Ibrahimovic ameshindwa  kubeba ndoo ya UEFA?
Mawazo ya kusema kuwa Ibrahimovic ni mchezaji wa game ndogo si kweli, kwani ameweza kuonesha uwezo mkubwa sana katika baadhi ya mechi kubwa ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Kwanza kabisa Ibrahimovic ni mshambuliaji wa kipekee katika bara la Ulaya kutokana na aina yake ya uchezaji ni mchezaji ambaye wazungu humuita Penalty-box Player anakuwa hatari sana hasa timu inapokuwa inatengeneza nafasi nyingi ambazo yeye anafanya kazi rahisi tu ya kufunga.
Zlatan sio mzuri sana hasa linapokuja katika suala la kucheza mpira wa mashambulizi ya kushtukiza na hasa pale timu yake inapozidiwa hana msaada kwa sababau hana desturi ya kurudi nyuma na kusaidia kukaba, sasa ukizingatia hatua ya mtoanao ni michezo miwili tu amabayo huchezwa kiufundi zaidi basi ni dhahiri kwa Ibrahimovic na timu zake kutofanya vizuri katika hatua hizo za mtoano.
Kwa mfano ni rahisi sana kuona wachezaji kama Lionel Mesi, Cristiano Ronaldo, Frank ribery, Arjen Robben na Neymar kufanya mashambulizi ya kushtukiza “Counter attacking football” Lakini Zlatan siyo mchezaji wa aina hiyo.
Ameshinda magoli 8 katika michezo 37 ya hatua ya mtoano katika ligi ya mabingwa barani Ulaya ukilinganisha na magoli 38 aliyofunga katika michezo 79 ya hatua ya makundi ya ligi hiyo.
Sabau ya pili ni kwamba Ibrahimovic ni mbinafsi na anaendeshwa sana na mafanikio binafsi na kushinda Ligi ya mabingwa haihitaji ubafsi takwimu zinaonesha vilabu vinavyoshinda Ligi hiyo ni vile amabavyo vinacheza kitimu na vinapigana pamoja kama timu “Team Spirit”.
Zlatan sio aina ya mchezaji amabaye unaweza kujenga mashamulizi kupitia yeye kutokana na kutokuwa na tabia ya kushuka chini na kuanzisha mashambulizi ambayo kama timu inaweza kwenda na kupata magoli.
Kitendo cha Ibrahimovic kutopata mafanikio katika Ligi ya mabingwa Ulaya ni wazi kinaharibu hadhi yake licha ya mashabiki wa Serie A pamoja na wale wa Ligue 1 kunufaika na kiwango chake ambacho hakichuji kila mwaka lakini ni dhahiri kuwa Ligi hizo hazina ushindani mkubwa kama ilivyo kwa ligi nyingine barani Ulaya.




Source:Shaffihdauda.com














































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..