CCM yavamia ngome ya Mbowe, yachukua madiwani...

Madiwani waliojiuzulu, kutoka kushoto ni Diwani wa kata ya Weruweru, Machame Magharibi na Mnadani

Madiwani watatu wa CHADEMA katika jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro wamejiuzulu nafasi zao na kujiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi CCM, kwa maelezo kuwa wanamuunga mkono Rais Magufuli.
Madiwani hao ni Bw. Kiwili wa kata ya Weruweru, Bw. Kimaro wa Machame Magharibi ambaye pia alikuwa ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Hai na Evarist Kimathi wa kata ya Mnadani.
Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari baada ya kupokelewa na katibu wa itikadi na uenezi wa CCM taifa, Humphrey Polepole uliofanyika katika ofisi za CCM mkoa wa Kilimanjaro, madiwani hao wamesema kuwa wameridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na Rais Magufuli na hivyo wameona ni vema kuungana naye kuiletea maendeleo Tanzania wakiwa CCM.
Sababu nyingine iliyotajwa na madiwani hao ni migogoro ndani ya baraza la madiwani wanayodai kuwa inasababishwa na uongozi wa juu wa CHADEMA unaofanya chama kuwa ni mali ya mtu mmoja na kuminya demokrasia ndani ya chama.
Pia wamesema sababu nyingine ni kutelekezwa na mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ndiye mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freeman Mbowe, wakidai kuwa tangu uchaguzi umemalizika, mbunge huyo hajaonekana jimboni na kuwafanya wao kama madiwani kushindwa kumuwajibisha pale wanapoona jambo fulani la maendeleo halijafanyika.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Weruweru amekwenda mbali zaidi na kueleza kuwa siku zote amekuwa akihitaji kuwawajibisha watumishi wa TAMISEMI, lakini anashindwa kuwawajibisha akiwa chama tofauti na alichopo rais, ndio maana ameamua kujiunga na chama alichopo rais ili awe huru kuwawajibisha.
Kwa upande wake Polepole amewaonya watu ndani ya chama wanachotoka madiwani hao kutowadhuru wanachama hao wapya wa CCM huku akisisitiza kuwa lengo la chama hicho ni kuhakikisha Dkt. Magufuli anashinda kwa asilimia zaidi ya 75 katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.


Source:Azamtv



































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..