Kiongozi wa upinzani Leopoldo Lopez aachiliwa Venezuela..
Rais wa Venezuela Nicolás Maduro amepongeza hatua ya kumuachilia kutoka gerezani moja wa viongozi wakuu wa upanzani nchini humo Leopoldo Lopez.
Bwana Lopez amepelekwa katika kifungo cha nyumbani baada ya kukaa gereza kwa zaidi ya miaka mitatu.
Aliondoka gerezani karibu na mji wa Caracas na kujiunga na familia yake siku ya Jumamosi.
Bwana Lopez alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 14 kwa kuchochea ghasia wakati wa maandamano ya kuipinga serikali mwaka 2014, mashtaka ambayo ameyakanusha. Mahakama kuu inasema kuwa ameachiliwa kwa misingi ya kiafya.
Bwana Maduro alisema kuwa anaunga mkono na kuheshimu uamuzi wa mahakama lakini lakini akataka kuwepo kwa amani.
Saa chacahe baada ya kuichiliwa Bwana Lopez aliwashauri wafuasia wake kuendelea kuandamana barabarani kumpinga Bwana Maduro.
Akielezea maisha ya mwawawe gerezani babake Lopez aliiambia radio moja ya Uhispania siku chache zilizopita kuwa aliadhibiwa kwa kufungiwa katika chumba kisicho na mwangaza na maji kwa muda wa siku tatu.
Alisema kuwa mwamawe sasa alikuwa amefungiwa kifaa cha eletroniki ili mamlaka ziwezi kufuatilia mienendo yake.
Lopez alipigwa picha akishika bendera ya Venezuela
Source:BBC
Maoni
Chapisha Maoni