Israel yaondoa hatua zote za kiusalama mjini Jerusalem..
Hatua zote za kiusalama zilizoweka hivi majuzi mjini Jerusalem, zilizozua maandamano kutoka kwa wapalestina zimeendolewa kwa mujibu wa polisi nchini Israel.
Viongozi wa dini katika utawala wa Palestina sasa wataacha kususia eneo hilo takatifu.
Vizuizi hivyo viliendelelea leo asubuhi, siku mbili baada ya mitambo wa kutambua chuma kuondolewa.
Mzozo uliibuka baada ya kuliwa kwa polisi wawili wa Israel karibu wiki mbili zilizopita.
Israel imesema kuwa itachukua hatua zisizokuwa na vizuizi miezi sita inayokuja.
Kumekuwa na karibu makabiliano ya kila siku kati ya vikosi vya usalama vya Israel na waandamanaji tangu mitambo ya kutambua chuma iwekwe baada ya kuuwawa kwa polisi tare 14 mwezi huu karibu na eneo linalofahamika kama Haram al-Sharif kwa waislamu na Temple Mount kwa wayahudi.
Wapalestina wanne waliuawa na raia watatu wa Israel kuuliwa kwa kuchomwa visu na mpaletina ambaye alidai alikuwa akilipiza hatua za Israel eneo takatifu.
Viongozi wa dini katika utawala wa Palestina sasa wataacha kususia eneo hilo takatifu.
Source:BBC
Maoni
Chapisha Maoni