Mlima Oldonyo Lengai wakaribia kulipuka, wanasayansi waonya..

Muonekano wa mlima Oldonyo Lengai 'Mlima wa Mungu' picha na Daily Mail

Mlipuko mkubwa wa volkano huenda ukatokea hivi karibuni kwenye mlima Oldonyo Lengai uliopo mkoani Arusha Tanzania.
Wataalamu wameonya kuwa mlipuko huo unaweza kusambaa nje ya eneo hilo lenye historia kubwa kuhusu mwanadamu.
Mlima huo unaotajwa kuwa na volkano hai, una urefu wa futi 7,650, kutoka usawa wa bahari, ambapo upo umbali wa chini ya maili 70, kutoka sehemu iliyogundulika kuwepo unyayo wa mtu wa kale ambao uliachwa zaidi ya miaka milioni tatu na nusu iliyopia.
Pia mlima huo upo karibu kabisa na eneo ambalo nyayo 400 za binaadamu ziligunduliwa na wanasayansi miaka 19,000, iliyopita.
Watafiti wanaosomea masuala ya mitikisiko ya volkano, wameonya kwamba mlipuko huo unaweza kutokea muda wowote kuanzia sasa na kuharibu moja kwa moja sehemu muhimu za kihistoria.
Jina Oldonyo Lengai linatokana na lugha ya kimasai, maana yake ni ‘mlima wa Mungu’. Inadaiwa kuwa jina hilo limetokana na tabia ya kabila hilo kwenda kufanya matambiko na kuupa sifa ya uungu.



Source:AzamTv



























































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..